ABSTRACT

This chapter draws on the authors’ collective experiences of social work education and knowledge mobility as social work students, researchers, and educators in three countries in the Global North. It discusses knowledge transfer through four channels: social work education, research, academic publication, and digital information-sharing platforms. It promotes co-constructed knowledge sharing to facilitate decolonisation and recommends a review of social work curricula globally to ensure they examine the origins of knowledge taught in light of the international definition's thrust towards local and cultural relevance and the Global Agenda's embrace of Ubuntu in its first theme to strengthen social solidarity and global connectedness. In so doing, it recommends the inclusion of indigenous teaching methods, knowledge, and research frameworks to foster social work's engagement with Indigenous Peoples’ issues, noting a premier role for the profession's international education body in leading the decolonising thrust in social work education.

Waandishi wameandaa sura hii kutokana na uzoefu wao wa pamoja wa elimu ya ustawi wa jamii na uhamishaji wa maarifa kama wanafunzi, watafiti, na watoaji elimu ya ustawi wa jamii katika nchi tatu zilizopo Kaskazini mwa dunia. Inajadili uhamishaji wa maarifa kupitia njia nne: elimu ya ustawi wa jamii, utafiti, machapisho ya kitaaluma, na majukwaa ya kidijitali ya kupeana habari. Inakuza kushirikishana kwa maarifa yaliyojengwa kwa pamoja ili kuwezesha kuondoa ukoloni inapendekeza uchunguzi wa mitaala ya ustawi wa jamii duniani kuhakikisha inachunguza asili ya maarifa yanayofundishwa kwa kuzingatia ufafanuzi wa kimataifa kuelekea umuhimu wa kitamaduni na Agenda ya Kimataifa kukumbatia Ubuntu katika mada yake ya kwanza kuimarisha mshikamano wa kijamii na muunganisho wa kimataifa. Kwa kufanya hivyo, inapendekeza kujumuishwa kwa njia za asili za kufundisha, maarifa, na mifumo ya utafiti ili kukuza ushirikiano wa ustawi wa jamii na masuala ya watu wa asili, kwa kubainisha jukumu kuu la shirika la elimu ya kimataifa la taaluma hiyo katika kuongoza msukumo wa kuondoa ukoloni katika elimu ya ustawi wa jamii.